
Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Edward Lowassa Leo anatarajiwa kuchukua fomu ya Urais katika tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC
Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na chama hicho Lowassa atachukua fomu saa tatu asubuhi huku skisindikizwa na viongozi mbalimbali wa vyama hivyo pamoja na Wanachama Msafara ukitarajiwa kuanzia ofisi za CUF, Buguruni.
Akizungumza jana Baada ya kutembelea Wanachama wa CUF, ofisini kwao Mh. Lowassa amewataka wanachama wa chama hicho kushikama na kuonyesha umoja ikiwa ni pamoja na kujitokeza kupiga kura ili waweze kupata ushindi wa Kishindo.
Wakizungumza katika Mkutano huo viongozi mbalimbali wa Umoja huo wamesema kuwa mshikamano ni jambo la umuhimu na kusema lengo lao la kukota chama tawala litatiamia endapo watashikama kwa dhati.