
Katika taarifa yake, Kamishna Ufundi na Mipango wa Shirikisho la Kikapu Tanzania TBF Manase Zabron wamepokea mwaliko wa kuwasafirisha wachezaji wawili ambao watakaa kwa muda wa wiki moja kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali yanayohusiana na mpira wa kikapu yaliyoandaliwa na Shirikisho la Mpira wa kikapu Duniani FIBA.
Manase amesema, wanawachezaji wengi lakini wameweka vigezo ambavyo wanaamini kabisa watawapata wachezaji wawili watakaokwenda kuwakilisha nchi ipasavyo.
Manase amesema, wameshaanza mchakato wa kusambaza barua kwa timu zote ili waandae wachezaji wao ambao watawashindanisha na kupata idadi inayotakiwa.