Ijumaa , 31st Jul , 2015

Azama ya Tanzania na Gormahia ya Kenya zitakutana katika fainali ya klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati maarufu Kagame Cup siku ya jumapili baada ya timu hizo kushinda kwenye michezo yao ya nusu fainali hii leo.

Kikosi cha Azam kilichotinga fainali ya kombe la Kagame 2015.

Azama ya Tanzania na Gormahia ya Kenya zitakutana katika fainali ya klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati maarufu Kagame Cup siku ya jumapili baada ya timu hizo kushinda kwenye michezo yao ya nusu fainali hii leo.

Azam imeingia hatua hiyo ya fainali mara baada ya kuifunga KCCA ya Uganda kwa jumla ya bao 1-0 kwenye mchezo wa pili uliopigwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa,mfungaji wa bao la Azam akiwa Faridi Mussa akiunganisha krosi safi ya Ame Ally dakika ya 77.

Nayo GOR Mahia ya Kenya imetinga fainali hiyo baada ya kuifunga Khartoum ya Sudan kwa jumla ya mabao 3-1 kwenye mchezo wa kwanza ulipigwa mchana wa leo kwenye uwanja huo huo wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mabao ya Gor Mahia leo yamefungwa na Michael Olunga kwa penalti, Innocent Wafula na Meddie Kagerem, wakati bao pekee la Khartoum limefungwa na Amin Ibrahim Elman.