Jumapili , 5th Jul , 2015

Kampuni ya uchimbaji madini ya Geita Gold Mine (GGM) inakusudia kukusanya zaidi ya sh.Bilioni 1 za kitanzania toka kwa mashirika na wadau mbalimbali wa Maendeleo zitakazosaidia mapambano dhidi ya ugonjwa wa ukwimi na kuboresha miradi ya afya ,elimu.

Makamu wa Rais wa kampuni ya Geita Gold Mine barani Afrika Simon Shayo

Makamu wa Rais wa kampuni ya Geita Gold Mine barani Afrika Simon Shayo aliyasema hayo jana katika taaarifa yake kwa Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro wakati wanaharakati wapatao 39 kutoka nchi mbali mbali ulimwenguni wakiwemo watoto wawili kutoa kituo cha watoto yatima cha moyo wa huruma waliungana na kampuni GGM katika kampeni kupanda milima Kilimanjaro kwa lengo la kupambana na ugonjwa hatari wa Ukimwi.

Alisema GGM,ilianzisha kampeni ya kukusanya fedha kwa ajili ya kusaidia waathirika wa ugonjwa wa ukimwi tangu mwaka 2002 na kwamba kila mwaka wamekuwa wakikusanya zaidi ya shilingi milioni mia nane kwa ajili ya kusaidia waathirika na kupambana na ugonjwa wa Ukimwi,

Shayo alisema mwaka huu kampeni hiyo inakusudia kukusanya zaidi ya shilingi bilioni moja na milioni mia tano na kwamba fedha hizo wanazichangisha toka makampuni mbali mbali na kuzipeleka fedha hizo kwa mashirika yasiyokuwa na fedha yanayopambana na ugonjwa wa ukimwi .

Alisema ni miaka takriba ni kumi na mine toka kampuni ya GGM ,ianzishe kampeni ya kupanda mlima Kilimanjaro kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kupambana na ukimwi na kuwa kampeni hiyo kwa kushirikiana na wadau mbali mbali ikiwemo serikali na mataifa mengine imeanza kuleta mafanikio makubwa dhidi ya mapambano ya ugonjwa huo kutokana na maambukizi ya ugonjwa huo kupungua hapa nchini.

Awali akimwakilisha Mwenyekiti wa tume ya kupambana na ugonjwa wa ukimwi TACAIDS,Mkurugenzi wa ufuatiliaji na tathimini toka tume ya TACAIDS Dr.Jerome Kamwela alisema maambukizi ya ukimwi yamepungua hapa nchini na kwamba mwaka 2000 maambukizi kwa watu waliokuwa na umri kati ya miaka 15 hadi 49 yalikuwa 150,000 lakini hivi sasa yameshuka hadi 75,000 kwa mwaka sawa asilimia 5.3.

Alisema TACAIDS na wanakusudia kutoa misaada kwa vituo vya watoto yatima na kutoa elimu ya kupambana na ukimwi kwa madereva wa safari ndefu katika mikoa mbali mbali hapa nchini ili kuweza kupunguza ama kumaliza maambukizi ya ukimwi hadi kufikia asilimia sifuri.

Akizindua kampeni ya kupanda mlima huo kupitia kampuni ya GGM,Katibu tawala mkoani Kilimanjaro kwa niaba ya mkuu wa mkoa Kilimanjaro Severine Kahitwa aliipongeza kampuni ya GGM,kwa kutumia zaidi ya shilingi bilioni kumi kwa ajili ya kuboresjitihada za barabara,maji,elimu na afya mkoani Geita ikiwa ni pamoja na jitihada za kupambana naugonjwa wa ukimwi.

Alimpongeza Rais Ally Hassani Mwinyi,Benjamini Mkapa na Rais Jakaya Kikwete kwa jitihada zao za kupamba na ugonjwa wa ukimwi hapa nchini na kudai jitihada hizo hazina budi kuungwa mkono na kila mwananchi ili kuweza kutokomeza maambikizi ya ugonjwa wa ukimwi hapa nchini.