Ijumaa , 3rd Jul , 2015

Producer C9 kutoka C 9 Records, baada ya harakati za kuunganisha wasanii kutoka Ruvuma kuwaendeleza kwa kazi za pamoja, mpango alioupatia jina 'Bwela Kuni' ameweka wazi kukwamishwa kwa harakati hizo na mkuu wa mkoa wa Ruvuma.

mtayarishaji wa muziki nchini Tanzania C9 Kanjenje

Nyota huyo amesema kuwa project hiyo kubwa alioutambulisha na washirika wake mwaka jana, mpaka sasa hawajaamua kuchukua hatua nyingine kutokana na kuepusha kwenda tofauti na uongozi wa Serikali katika shughuli ambayo pia inahusisha uongozi wake moja kwa moja kama anavyoeleza hapa.

Kwa upande mwingine C9 ameeleza pia juu ya kurejea katika utayarishaji wa Bongo Flava baada ya kujikita katika Dansi na Taarab kwa muda.