Jumanne , 30th Jun , 2015

Mtayarishaji muziki na mwimbaji wa Bongofleva, Bob Junior ametoa dongo kwa watayarishaji muziki wasiojua kuimba na kuwachana bila kuzungusha maneno kuwa watayarishaji wa aina hiyo hawazifahamu vizuri ala za muziki.

msanii wa miondoko ya bongofleva nchini Bob Junior

Bob Junior amesema kuwa, mtayarishaji muziki aliyekamilika anatakiwa kufahamu kuimba na vilevile kupiga kinanda na ikiwa ni vinginevyo basi kwa upande wake moja kwa moja anaona kunakuwa na tatizo kwa upande huo.

Kwa upande wa pili, Sheddy Clever, moja ya watayarishaji muziki ambao hawaimbi, amesema kuwa kwa upande wake ameona kushikilia mambo mawili kwa wakati mmoja ni kujichanganya tu.