Kocha mkuu wa Stars Mkwasa akizungumza na waandishi wa habari
Katika taarifa yake, Mkwasa amesema, tayari kikosi hicho kipo kambini Bagamoyo kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa marudiano dhidi ya Uganda.
Mkwasa amesema, kikosi chake kimeingia kambini ambapo kimemkosa kiungo Jonas Mkude ambaye amesafiri kuelekea nchini Afrika Kusini kwa ajili ya majaribio ambapo amesema kuwa anaamini Mkude atafanikiwa kwani ameenda kutafuta maisha.
Mkwasa amesema, kikosi alichokichagua kina mwonekano mpya hivyo mpaka hapo hakuna mchezaji mwenye uhakika wa namba hivyo kila mchezaji anatakiwa kujituma ili kuhakikisha anapata nafasi ya kucheza katika kikosi hicho.