Jumanne , 20th Aug , 2024

Shirikisho la soka Duniani FIFA limeiamuru timu ya Yanga inayoshiriki ligi kuu ya NBC kuilipa kiasi cha dola za Marekani 80,000 ambazo ni zaidi ya milioni 200 kwa shilingi ya Tanzania klabu ya Bechem United ikiwa ni ada ya uhamisho wa Mghana Augustin Okrah aliyejiunga na klabu hiyo

Barua kutoka FIFA imeeleza kuwa Yanga wanatakiwa kulipa kiasi hicho ndani ya siku 45 kutoka Agosti 19 au kukata rufaa kabla ya Septemba 3 2024 endapo hawajakubaliana na hukumu hiyo

Okrah ambaye alitambulishwa na Yanga  kwenye michuano ya Mapinduzi 2024 na ameachana na klabu hiyo Julai 2024 baada ya mkataba wake kumalizika huku  alisaini mkataba wa mwaka mmoja na Bechem United  Septemba 7 2023 baada ya kuachana na Simba SC Julai 2023