Jumanne , 26th Jul , 2022

Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Klabu Ya Yanga, Hassan Bumbuli amethibitisha kuwa asilimia tisini ya Wachezaji wa Klabu hiyo wapo kambini na wameanza mazoezi ya kujiandaa ya msimu ujao isipokuwa kwa Mchezaji Bernard Morrison anayetaraji kuwasili nchini Jumatano hii.

Bernard Morrison

Yanga tayari wameanza mazoezi ya kujiweka fiti kujiandaa na msimu mpya wa ligi sambamba na mashindano ya kimataifa wakiiwakilisha nchi Klabu bingwa.

Ofisa Habari wa klabu hiyo, Hassan Bumbuli amesema  wachezaji wote wamewasili kambini isipokuwa Bangala na Morrison ambao hadi alhamisi watakuwa wameungana na wenzao kwenye mazoezi.

"Mastaa hao taarifa za kuchelewa kwao zinafahamika lakini wote watawasili kesho na alhamisi wataanza mazoezi pamoja na wenzao ili kujiweka witi kuelekea msimu mpya," alisema na kuongeza;

"Ni wachezaji watano ambao walichelewa kujiunga na kambi ambao ni Khalid Aucho ambaye jana kaanza mazoezi, Fiston Mayele na Shaban Djuma ambao wataanza mazoezi leo baada ya kuwasiri jana."