Akiongea na EATV kocha wa Viungo Hussein Bunu amesema kuwa wachezaji wote wapo vyema na wanaendelea na mazoezi huku kila moja akijua malengo yao nikukaa katika nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi kuu katika msimu 2023 - 2024.
“Tumeanza rasmi mazoezi Leo wachezaji wote tupo nao hatujawapa mapumziko hivyo tunatambua ni mchezo mgumu kutoka na wapinzani wetu Coastal Union kutokuwa na matokeo mazuri katika michezo hii ya awali”amesema Bunu.
kwa upande wake Msemaji wa Klabu hiyo Hamis Milyango amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi katika mchezo huo kuja kushuhudia namna ambavyo wanacheza soka la mipango .
“Mashujaa FC tumepanda Ligi kuu kuja kuwaonyesha klabu namna ambavyo tunacheza soka la kuvutia na Yoyote atayekuja katika uwanja wa Nyumbani Kigoma hawezi kutoka Salama “Milyango amesema .
Nae nahodha wa klabu hiyo Saidi Makapu amesema kutokana na mazoezi wanayopatiwa kila siku watajitahidi kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye michezo yao ili wabakie ligi kuu na hata pia kupata nafasi ya kuiwakilisha nchini katika michuano ya Ligi ya Mabingwa na Shirikisho barani Afrika .
katika msimamo wa Ligi kuu NBC Tanzania kikosi cha Mashujaa FC kutoka Kigoma kinashika nafasi ya tano kikiwa na alama zake nane huku kinara wa akiwa Simba SC na pointi zake 15 na Coastal Union akishika mkia na alama zake 2.