Jumanne , 10th Sep , 2024

Mwili wa Wilhelim Gidabuday utapumzishwa kwenye nyumba yake ya milele Jumamosi kijijini kwao Nangwa, Katesh.
Gidabuday aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Shirikisio la Riadha Tanzania (RT), amefariki alfajiri ya kuamkia jana Septemba 10, 2024 baada ya kugongwa na gari jijini Arusha.

Mdogo wa marehemu, Julius Gidabuday amesema  safari ya kwenda Katesh mkoani Manyara itaanza Ijumaa jioni na Jumamosi kaka yake atazikwa.

Hadi mauti yanamkuta, Gidabuday alikuwa katibu wa Kamati ya Mabadiliko ya Katiba ya RT, ambayo ilikuwa inaelekea ukingoni kukamilika.