Jumapili , 5th Mar , 2023

Mwanasheria wa Kiungo kutoka Zanzibar Feisal Salum ‘Fei Toto’ amesema ni mapema mno kuzungumza lolote kwa sasa, kufuatia maamuzi yaliyotangazwa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’.

Fatma Karume ambaye alikuwa sehemu ya Wanasheria wa Kiungo huyo

Feisal aliomba kurejewa kwa maamuzi ya shauri lake dhidi ya Young Africans, lakini bado Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ikaendelea kusimamia msimamo wake wa kumtambua kama Mchezaji halali wa Klabu hiyo ya Jangwani.

Fatma Karume ambaye alikuwa sehemu ya Wanasheria wa Kiungo huyo katika marejeo ya Shauri la Feisal dhidi ya Young Africans jana Alhamis (Machi 02), amesema wanachosubiri kwa sasa ni nakala ya hukumu ili taratibu nyingine zifuate ikiwa pamoja na kumshauri mteja wake.

Amesema jambo kubwa na la msingi katika kesi hiyo, ni mteja wake kulazimishwa kuendelea kuitumikia Young Africans, ili hali yeye mwenyewe hataki kufanya hivyo, na TFF kupitia Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji wanapaswa kuzingatia suala hilo.

“Tunasubiri nakala ya hukumu kutoka TFF na kisha nitamshauri Fei Toto kama maamuzi yake yatabaki hivyo tutaenda CAS.”