
Beki wa kushoto wa Yanga, Yassin Mustapha
Mustapha hakuwa na msimu mzuri Yanga na mara nyingi benchi la ufundi la Yanga lilikuwa likiwapa nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza Farid Musa ama Kibwana Shomari.
Wakala wa Mchezaji huyo, Alison Mwaliwale amesema Mustapha tayari amesaini mkataba wa miaka wiwili kuichezea timu hiyo na kinachosubiriwa ni kumtangaza.
Amesema mkataba wa Yanga na Mustapha unaisha Julai 30 mwaka huu na baada ya hapo atakuwa Mchezaji huru.
"Tumemaliza hakuna chochote anachodai Yanga na Singida bado ni kumtangaza tu ila Yassin ni mali ya Singida Big Stars kwa sababu Yanga wao wamekubali kila kitu kiwekwe wazi hata kabla ya tarehe 30," Amesema Mwaliwale.
Wachezaji ambao tayari wamemwaga wino kuichezea timu hiyo ni mabeki, Paul Godfrey ‘Boxer’ kutokea Yanga na ‘AbdulMajid Mangalo aliyekuwa nahodha wa Biashara United.