
Simba na RS Berkane kwa Mkapa.
Katika mechi hizo za Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika, nchini Morocco mashabiki wa Berkane waliwatupia vitu wachezaji wa Simba Uwanja wa Manispaa ya Berkane, Februari 27, mwaka huu wenyeji wakishinda 2-0 na kwa kosa hilo wametozwa faini ya dola 8,000.
Na kwenye mchezo wa marudiano Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam, wenyeji Simba wakiibuka na ushindi wa 1-0 Machi 13, Makamu wa Rais wa Berkane, Majjid Madrane alivamia uwanjani na kuwaongoza wachezaji wake kuwafanyia fujo marefa.
Kwa kosa hilo, Kamati ya Nidhamu ya CAF kwanza imemfungia Majid Madrane kujihusisha na shughuli zozote za soka zinazotambauliwa na bodi hiyo ya kandanda barani kwa mwaka mmoja pamoja na kumpiga faini ya dola za Kimarekani 100,000.