Jumatano , 23rd Feb , 2022

Mchezaji namba 3 kwa ubora katika mchezo wa tenisi duniani na bingwa wa Olympic Alexander Zverev ameondolewa katika michuano ya Mexican Open baada ya kuipigiza raketi yake na kuigonga miguu ya mwamuzi huku akitoa lugha chafu za matusi akimlaumu msimamizi huyo kwamba ameharibu mchezo.

(Alexander Zverev akiondoka uwanjani)

Zverev raia wa Ujerumani amefukuzwa kwenye michuano hiyo ya wazi ya Mexico kwa kitendo cha kugonga kiti na miguu ya mwamuzi huyo akiwa anarudi kukaa kwenye kiti chake baada ya mchezo kumalizika na kupigiza raket yake mara tatu kwa nguvu na hasira katika miguu ya mwamuzi anayekaa juu katikati ya uwanja usawa wa wavu baada ya kufungwa seti mbili kwa alama 6 - 2, 4 - 6, na 10 - 6 dhidi ya Lloyd Glasspool.