Kocha wa muda wa Real Madrid akizungumza na mara baada ya uteuzi wake hapo jana.
Zidane ambaye aliichezea kwa mafanikio klabu hiyo tangu atue Santiago Bernabeu mwaka 2001 hadi 2006 kwa ada ya rekodi ya dunia kipindi hicho ameteuliwa hapo jana baada ya kutimuliwa kwa aliyekuwa kocha mkuu Rafael Benitez .
Benitez alitimuliwa baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa miezi saba pekee katika mkataba wake wa miaka mitatu huku akionekana kushindwa kukidhi kiu ya mashabiki na uongozi wa klabu kutokana na aina ya soka wanalocheza.
Kibarua cha Zidane kitaanza rasmi kwenye mechi dhidi ya Derpotivo la Coruna huku kocha huyo akiangaziwa kufuta machungu ya vipigo katika mechi kubwa ikiwemo El Classico dhidi ya Fc Barcelona.