Ijumaa , 29th Mar , 2019

Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera amezungumzia juu ya mipango ya usajili ya klabu hiyo kuelekea msimu ujao wa ligi pamoja na tetesi zinazoendelea kusambaa juu ya wachezaji wake kutakiwa na klabu zingine.

Kocha Mwinyi Zahera

Akizungumza na www.eatv.tv kutoka jijini Mwanza ambako Yanga inatarajia kucheza mchezo wa robo fainali Kombe la Shirikisho dhidi ya Alliance FC wikiendi hii, Zahera amesema kuwa amesikia tetesi za wachezaji wake kutakiwa na vilabu vingine lakini yeye haogopi chochote.

"Watu wengi wananipigia simu kuniambia kua wachezaji wa Yanga wengi wanatakiwa na timu zingine, mfano Kevin, Tshitshimbi, Feisal lakini mukiangalia mechi nyingi tumecheza bila wao na tunashinda. Yanga leo hakuna mchezaji hata mmoja ambaye akikosekana kwenye timu yetu tutakosa amani, sina hata mchezaji mmoja ambaye nitakosa usingizi sababu akiondoka", amesema Zahera. 

Zahera aitaja tarehe ya kumaliza usajili Yanga

 

"Mimi Zahera Mwinyi niliwaambia viongozi kuwa msiogope kwa kuwa wachezaji fulani wanatakiwa na timu zingine kwa sababu ni za uongo. Muwaache wote wanaotaka kuondoka na mtajionea baada ya miezi miwili ijayo timu itakavyokuwa kutokana na usajili nitakaoufanya. Mimi nataka kumaliza usajili wangu tarehe 15 mwezi wa 5 kwasababu Juni Mosi ninasafiri kwenda kambi ya timu ya taifa Ulaya", ameongeza.

Pia kocha huyo ameitaja sababu ya kuwatema wachezaji Ibrahim Ajib, Mo Banka, Mwinyi Haji na Juma Abdul katika kikosi kilichosafiri Mwanza kuwa ni baada ya kuchelewa mazoezi ya siku mbili kabla ya safari hiyo.

Bonyeza hapa chini kutazama zaidi.