Jumamosi , 14th Sep , 2019

Kocha wa klabu ya Yanga Mwinyi Zahera, amesema kuwa licha ya uzoefu wa Zesco katika michuano ya Ligi ya Mabingwa lakini watahakikisha wanawafunga leo.

Kocha Mwinyi Zahera

Akiongea kuelekea mchezo huo Zahera amesema kuwa, wanatambua Zesco ni wazoefu kuliko Yanga lakini amepata usaidizi wa mbinu zo kutoka kwa kocha wa TP Mazembe, Pamphile Mihayo Kazembe hivyo watakabiliana nao.

Yanga inacheza na Zesco leo Septemba 14, 2019 kwenye uwanja wa Taifa Dar es salaam ikiwa ni raundi ya pili ya hatua za awali ambapo mshindi wa jumla katika mechi mbili ataingia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Zaidi tazama kwenye video hapo chini.