Jumapili , 6th Aug , 2017

Beki wa pembeni wa Taifa Stars, Gadiel Michael amesaini rasmi mkataba wa miaka miwili kujiunga na Mabingwa wa ligi kuu Tanzania Bara Yanga SC, baada ya uongozi wa Azam FC, kufikia makubaliano na klabu hiyo ya Jangwani.

                               Mchezaji mpya wa Yanga, Gadiel Michael

Wakati huo huo uongozi wa Azam FC kupitia msemaji wa timu hiyo Jaffar Iddi Maganga wamewashukuru viongozi wa Yanga kwa kuwa waungwana na kufika kwenye ofisi zao wakiongozwa na mwenyekiti wa usajili, Hussein Nyika.

"Tumewapunguzia bei imekuwa nusu yake na taratibu zote zimekamilika baada ya pande zote kukubaliana ni rasmi sasa, tunathibitisha ni ruksa kwa Yanga kumsajili Gadiel kwa msimu ujao na tunamtakia kila la kheri katika maisha yake mapya ndani ya timu hiyo", amesema Maganga.

                                       Msemaji wa timu ya Azam Fc, Bwana. Jaffar Iddi Maganga

Kwa upande mwingine, Maganga amesema siyo jambo la kweli kuwa wachezaji wakitaka kuenda klabu ya Simba huwa wanaenda bure ila kwa yanga wanabaniwa kama baadhi ya watu wanavyoeneza uvumi huo.