Jumatatu , 20th Sep , 2021

Kikosi cha mabingwa wa kihistoria wa Tanzania bara Yanga SC kimerejea nchini leo Asubuhi kikitokea nchini Nigeria ambako kilicheza mchezo wa klabu bingwa Afrika hatua ya awali dhidi ya Rivers United mchezo ambao Yanga ilifungwa 1-0 na kutupwa nje ya mashindano.

Wachezaji wa Yanga wakiwa uwanja wa Ndege

Kipigo hicho kimeifanya Yanga itupwe nje ya mashindano ya klabu bingwa kwa kipigo cha jumla cha mabao 2-0, kwenye michezo miwili wa ugenini na nyumbani, timu hiyo ya wananchi imepoteza michezo yote miwili kwa kufungwa bao 1-0. Kikosi cha Yanga kimerejea na msafara wa watu wote 60 ambao umejumuhisha wachezaji, viongozi na baadhi ya mashabiki.

 

Na kwa mujibu wa ripoti kutoka ndani ya Yanga zinadai kuwa timu hiyo ya wananchi ilikumbana na vitendo visivyo vya kiungwana yani figisu kutoka kwa wenyeji wao, ikiwemo kucheleweshewa majibu ya vipimo vya Uviko 19 na baadae wachezaji wao wanne kutajwa kuwa na Uviko 19 ambao ni Fei Toto, Mukoko Tonombe, Djdgui Diarra na Yacuba Sogne ingawa wachezaji wote hawa walicheza lakini pia Yanga hawakutumia vyumba rasmi vya kubadilishia nguo na badala yake walitumia sehemu ya benchi la kukaa makocha na wachezaji wa akiba uwanjani kama seheumu ya kubadilishia nguo.

Mara baada ya kutupwa nje ya michuano hiyo kikosi cha Yanga kinajikita zaidi kwenye michezo ya Ligi Kuu Tanzania bara na kombe la Azam Sports Federation Cup  na mchezo wao wa mashindano unaofata ni dhidi ya watani zao Simba SC mchezo wa ngao ya Jamii utakao chezwa Septemba 25 katika Dimba la Benjamini Mkapa Da es salaam.