Jumapili , 3rd Nov , 2024

Klabu ya Yanga jana imepoteza kwa mara ya kwanza mchezo wa ligi kuu Tanzania bara kwa kufungwa goli 1-0 dhidi ya Azam SC huo mchezo uliochezwa uwanja wa Azam Complex Chamazi Dar es salaam. Goli la Wahoka Mikate tokea Chamazi liliwekwa kimiani na nyota wa kimataifa wa Gambia Gibril Sillah.

Kikosi cha Wanajangwani kimesalia na alama zake 24 bado kikiwa kinaongoza msimamao wa ligi kuu Tanzania bara, Singida Black Stars inashika nafasi ya ya pili ikiwa na alama 23 na Simba SC yenye alama 22 ipo nafasi ya 3 baada ya timu za Kariakoo kucheza michezo 9 kila moja Singida Black Stars imecheza michezo kumi ya ligi mpaka sasa.

Klabu ya Yanga jana imepoteza kwa mara ya kwanza mchezo wa ligi kuu Tanzania bara kwa kufungwa goli 1-0 dhidi ya Azam SC huo mchezo uliochezwa uwanja wa Azam Complex Chamazi Dar es salaam. Goli la Wahoka Mikate tokea Chamazi liliwekwa kimiani na nyota wa kimataifa wa Gambia Gibril Sillah dakika ya 33 ya mchezo.

Kikosi cha Wanajangwani kimesalia na alama zake 24 bado kikiwa kinaongoza msimamao wa ligi kuu Tanzania bara, Singida Black Stars inashika nafasi ya ya pili ikiwa na alama 23 na Simba SC yenye alama 22 ipo nafasi ya 3 baada ya timu za Kariakoo kucheza michezo 9 kila moja Singida Black Stars imecheza michezo kumi ya ligi mpaka sasa.

Azam SC ilistahili kupata mkwaju wa penati baada ya Mchezaji wake Pascal Gaudence Msindo kuchezewa madhambi na kiungo wa Yanga SC Mudathir Yahya  kwenye eneo la hatari Refarii Ahmed Arajiga hakutoa adhabu ya mkwaju wa penati kwenye tukio hilo. 

Beki wa mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara Ibrahim Hamad Bacca hakumaliza mchezo baada ya kupewa kadi nyekundu na Muamuzi wa mchezo kwa kumzuia Mshambuliaji wa Wauza lambalamba kutoka Chamazi Nassor Hamoud aliyekuwa kwenye nafasi nzuri ya kuonana na Golikipa wa Yanga Djigui Diarra.

Bacca aliadhibiwa kwa kadi nyekundu kutokana na yeye kuwa Beki wa mwisho na kucheza faulo iliyomzuia Mshambuliaji kufunga kwa mujibu wa Sheria mpya kutoka International Football Association Board (IFAB) Bodi inayohusika na utungwaji wa sheria za soka Duniani.

Goli lililofungwa na Sillah siku ya jana linakuwa la kwanza kwa klabu ya Wananchi kuruhusu msimu huu kwenye michezo 10 iliyocheza. Kocha wa Yanga Muargentina Miguel Gamondi amemlalamikia Muamuzi wa mchezo kwa kusema tukio linalofanana na la kwao liliamuliwa tofauti mchezo dhidi ya Simba SC ambapo Prince Dube alichezewa faulo na Abdulrazack Mohamed Hamza lakini Refarii alitoa kadi ya njano badala ya nyekundu alionyesha kushangazwa Gamondi.

Ligi kuu Tanzania bara itaendelea tena leo na kesho Tanzania Prisons itacheza dhidi ya KenGold leo Novemba 3, 2024 uwanja wa kumbukizi ya Sokoine Jijini Mbeya. Mchezo huo unafahamika kwa jina la Mbeya Dabi kukokana na kuzikutanisha timu zote za kutoka Jiji hilo.

Kesho Novemba 4 kutakuwa na michezo ya ligi itakayochezwa viwanja tofauti Tabora United dhidi ya Mashujaa, Kagera Sugar dhidi ya Dodoma Jiji wakati mchezo uliokuwa uzikutanishe Namungo FC dhidi ya JKT Tanzania umeahirishwa kutokana na kikosi cha JKT kupata ajali kikiwa kinarejea Dar es salaam kutokea Dodoma kilipocheza mchezo wa ligi kuu dhidi ya Dodoma Jiji.