Akizungumza na Waandishi wa Habari ndani ya Makao Makuu ya Yanga mitaa ya Jangwani, Afisa habari wa Yanga SC Ally Kamwe amesema taarifa njema kwa sasa ni kurejea mazoezini kwa nyota Kibwana Shomari pamoja na Khalid Aucho huku bado Pacome Zouzoa,Yao Koussi Attouhola na Zawadi Mauya wapo chini ya uangilizi wa daktari mpaka sasa.
Aidha Ally Kamwe amesema Uongozi wa Yanga umeondoa kiingilio kwenye Jukwaa la Mzinguko kwenye mchezo dhidi ya Mamelodi Sundowns ili kutoa nafasi kwa mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo huo.
“Viongozi wa Klabu yetu hawana tamaa ya fedha, ndio maana tumepunguza a kuondoa tiketi ya mzunguko kwa lengo la kuhakikisha wengi waje Uwanjani. Tumeweka maslahi ya mpira wa Tanzania mbele. Mechi ya Mamelodi ni kubwa mno lakini kwa kuwa lengo sio fedha ni hamasa”amesema Kamwe
Kikosi cha Mamelodi Sundowns kinatarajiwa kuwasili nchini mnamo Machi 28-2024 kwa ajili ya mchezo wa mkondo wa kwanza wa robo fainali Ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Yanga SC utaopigwa majira ya Saa 3 Usiku kwenye dimba la Benjamin Mkapa.