Kikosi cha Yanga
Hafidh ameyasema hayo leo kuelekea mchezo wa ligi dhidi ya Singida United utakaopigwa kwenye dimba la Nanfua mjini Singida kuanzia saa 10:00 jioni.
''Bodi ya ligi wakati mwingine waangalie wanapopanga ratiba na ukiangalia usafiri wetu ni barabara kiukweli wachezaji wetu wanachoka, tumetoka Tanga kuja Singida kisha turudi tena Tanga kucheza mechi'', amesema.
Yanga ilicheza mchezo wake wa 21 wa ligi kuu msimu huu, Jumamosi iliyopita dhidi ya Coastal Union ambapo mechi hiyo iliisha kwa sare ya 1-1.
Yanga sasa ipo kileleni ikiwa na alama 54 wakati wapinzani wao wa leo Singida United wapo katika nafasi ya 13 ikiwa na alama 27.




