Jumatano , 12th Apr , 2017

Mabingwa wa Tanzania Bara Yanga SC kesho jioni wanatarajia kuondoka jijini Dar es salaam kuelekea nchini Algeria kupambana na MC Alger katika mchezo wa marudiano Kombe wa Shirikisho Afrika huku wakiwakosa wachezaji wake saba akiwemo Obrey Chirwa.

Wachezaji hao ni Justine Zulu, Malimi Busungu, Matheo Antony, Ally Mustapha, Pato Ngonyani, pamoja na Yusuph Mhilu hatua ambayo imetokana na baadhi ya wachezaji hao kuwa majeruhi.

Msafara huo umebeba benchi la ufundi na wachezaji wapatao 20 ambao ni  magoli kipa wake wawili ambaye ni Deogratus Munishi , Walinzi Nadir Haroub, Vincent Bossou, Juma Abdul, Andrew Vicent, Oscar Joshua, Mwinyi Haji, Hassan Ramadhani na Kelvin Yondani.

Viungo wanaokwenda na timu ni Thaaban Kamusoko, Haruna Niyonzima, Deus Kaseke, Said Juma Makapu, Juma Mahadh, Simon Msuva, Geofrey Mwashuiya pamoja na Emmanuel Martin.

Yanga ilitoka kifua mbele kwa bao 1-0 dhidi ya wapinzani wao, bao lililofungwa na Chirwa, katika mchezo wa kwanza uliopigwa katika dimba la Taifa Dar es Salaam.