
Aliyekua nahodha wa Yanga, Papi Kabamba Tshishimbi (Kulia katika picha), akimzuia kiungo machachari wa Simba Jonas Mkude (Kushoto Pichani) katika moja ya Dabi ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Tshishimbi ambaye aliibua zogo hivi karibuni baada ya kupishana na uongozi wa Yanga, anaachwa kutokana na mkataba wake kumalizika na hivi karibuni ilitaarifiwa kwamba hakukubaliana na ofa mpya aliyopewa huku akisisitiza kuongezewa maslahi makubwa.
Kupitia Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Mwanasheria, Patrick Simon alisema walimpatia ofa nahodha wao na hakuijibu , na wakampa siku 14 na iwapo asipoikubali basi wangeachana nae na wapo wachezaji bora zaidi yake na watawasaini hao kama mbadala.
Katika orodha ya wachezaji walioachwa yupo mshambuliaji kinara wa timu hiyo David Molinga kutoka Congo, na Patrick Sibomana raia wa Rwanda ambaye amesitishiwa mkataba wake.
Nyota wa kimataifa wa Ghana Benard Morrison amenusurika katika panga pangua hiyo huku wengi wakitafsiri kwamba lipo jambo nyuma ya pazia linaendelea dhidi ya winga huyo machachari asiyeishiwa vituko nje ya uwanja.
Aidha klabu hiyo imesema inafanya mazungumzo na nyota wake wakongwe Juma Abdul na Kelvin Yondan ambao mikataba yao ilishamalizika.
Katika kikao cha leo pia Yanga imeorodhesha majina ya wachezaji ambao hawatokuwepo katika kikosi chao kutokana na sababu mbali mbali.
Walioachwa baada ya mikataba yao kuisha
(1)Mrisho Ngasa
(2)David Molinga
(3)Jaffary Mohamed
(4)Tariq Seif
(5)Andrew Vincent Dante
(6)Papy Tshishimbi
(7) Mohamed Banka
Wanaoachwa kwa kusitishiwa mikataba Yao
(1)Ali Mtoni
(2)Muharami Issa
(3)Ali Ali
(4)Yikpe Gislain
(5)Patrick Sibomana
(6)Erick Kabamba
(7)Rapahael Daud
Waliopo kwenye mazungumzo kuongeza mkataba
(1)Juma Abdul
(2)Kelvin Yondan
Waliobaki Kikosini
(1)Farouk Shikalo
(2)Metacha Mnata
(3)Ramadhan Kabwili
(4)Haruna Niyonzima
(5)Lamine Moro
(6)Bernard Morrison
(7)Feiasal Salim
(8)Juma Mahadhi
(9)Adeyoum Saleh
(10)Said Juma Makapu
(11)Balama Mapinduzi
(12)Deus Kaseke
(13)Ditram Nchimbi
(14)Abdulaziz Makame
(15)Paul Godfrey.