
Akizungumza na East Africa Radio, Kocha msaidizi wa timu hiyo, Boniface Mkwasa amesema wameanza mazoezi wakiwa na wachezaji wachache kutokana na wachezaji wengi kuitwa katika timu zao za Taifa.
Mkwasa amesema, wameamua kuanza mazoezi mapema ili kuona uwezo wa wachezaji wapya ambao wanatarajia kuwasajili katika kikosi hicho pamoja na kujiweka tayari kwa ajili ya kushiriki michuano ya kombe la Kagame.