
Juu ni kikosi cha Simba na chini ni kikosi cha Yanga.
Mabadiliko hayo yemegusa mchezo namba 159, ambao unazikutanisha timu za Yanga SC dhidi ya Biashara United, ambao ulipangwa kuchezwa Jumapili Disemba 9, 2018 kwenye uwanja wa taifa saa 10:00 jioni.
Mchezo huo sasa utachezwa tarehe hiyo hiyo lakini imbedilishwa mudfa kutoka saa 10:00 jioni hadi saa 1:00 usiku kwenye uwanja huo huo wa taifa.
Mchezo mwingine ni ule wa kiporo kati ya Simba dhidi ya KMC, ambao umepangiwa tarehe na sasa utachezwa Jumatano ya Disemba 19 katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam saa 12:00 jioni.
Mchezo mwingine ni namba 170 kati ya KMC na TZ Prisons uliokuwa uchezwe Disemba 17, umerudishwa nyuma na sasa utachezwa Disemba 15 katika dimba la Uhuru kuanzia 10:00 jioni.