
Makundi ya michuano ya Mapinduzi ya Zanzibar iliyotolewa mapema na ZFA kwaka huu
Katika mchezo mwingine wa mapema wa kufuzu hatua ya nusu fainali, timu ya mafunzo imeichapa Azam FC 2-1 kwa ushindi usio na faida kwa timu hiyo baada ya kutupwa nje ya mashindano hayo kwa uchache wa pointi.
Yanga sasa watacheza nusu fainali na mshindi wa pili wa Kundi A huku Mtibwa Sugar nao wakikutana na mshindi wa kwanza wa kundi hilo.
Kundi A linamaliza mechi zake leo Ijumaa kwa Timu ya Jamhuri kuchuana na URA na Simba ikicheza na JKU huku kila timu ikiwa ina nafasi ya kutinga nusu fainali ikipata matokeo mazuri ingawa sare kwa Simba itawafikisha nusu fainali.
Timu za URA ya Uganda na Jamhuri ya Zanzibar zinahitaji ushindi wa hali na mali ili ziweze kufuzu .