Timu hiyo ya Jangwani itacheza na Mediama ya Ghana Desemba 8 au 9 ikianzia ugenini ambapo zitarudiana Desemba 18 au 19 kwenye uwanja wa Taifa.
Kundi hilo ambalo linatajwa kuwa kundi gumu zaidi, Yanga inatarajiwa kulipa kisasi kwa Mediama ambayo ilikuwa pamoja kundi D la Kombe la Shirikisho Afrika mwaka 2016.
Yanga na Medeama zinakutana tena katika Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.
Katika kundi hilo Yanga na Medeama zilishindwa kusonga mbele baada ya kumaliza katika nafasi mbili za mwisho.
Hii itakuwa ni nafasi nyingine kwa Yanga kulipa kisasi kwa Medeama ya Ghana kwani mwaka huo katika mchezo wa kwanza uliopigwa jijini Dar es Salaam Julai 16, 2016 ililazimishwa sare ya bao 1-1.
Katika mchezo wa marudiano uliopigwa Ghana wiki moja baadae ya Julai 26 mwaka huo, Yanga ilishindwa kutamba ilinyukwa mabao 3-1 na kuvuna pointi moja tu kati ya sita pindi ilipokutana na miamba hiyo.