
Serena Williams(kulia)na Maria Sharapova(kushoto) kwenye picha ya pamoja katika michuano ya wazi ya ufaransa mwaka 2013.
Williams anayeshikilia namba moja kwa ubora duniani aliumia goti na kujitoa kwenye mechi ya michuano ya Hopman Cup ambapo alikua nyuma kwa seti za 7-5, 2-1 dhidi ya Jarmila Wolfe huku mshindi mara tano wa Gland Slam Maria Sharapova akijiondoa kwenye mechi kutokana na maumivu ya mkono.
Kwa upande wake Williams anatarajiwa kutetea ubingwa wake alioutwaa mwaka jana nae Sharapova akiwania kurejesha heshima yake kwenye mashindano hayo mwaka huu.
Mashindano hayo makubwa yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi januari 18 hadi 31 huku nyota mbalimbali wa kiume na wa kike wakitarajiwa kuwania kinyanganyiro hicho.