Awali baraza hilo kupitia kwa katibu mkuu wake Ibrahim Akilimali lilitoa siku tano kwa manispaa ya Ilala kuwapa jibu juu ya ombi hilo vinginevyo wangefanya maandamano hayo makubwa kutokana na kile walichodai kuwa manispaa hiyo inawawekea kauzibe katika kufanikisha ujenzi wa uwanja wa kisasa wa timu hiyo kitu ambacho hawakukubaliana nacho
Lakini sasa kutokana na uongozi wa manispaa ya Ilala kuwaita nakuwaeleza kuwa suala lao litashughulikiwa haraka iwezekanavyo basi wao kwakuheshimu hilo wameamua kusitisha azma yao hiyo.