Jumapili , 30th Nov , 2014

Wazazi wametakiwa kuwajenga watoto katika michezo hususani mchezo wa karate ili kuweza kuwajenga kiakili na kiafya.

Akizungumza na East Africa Radio, kocha wa mchezo huo kwa vijana Jimson Malele amesema mchezo huo humsaidia mtoto kuwa na uwezo wa kufikiri katika masomo pia kumfanya kuwa na afya na kuondokana na maradhi mbalimbali.

Malele amesema michezo humsaidia mtoto kumpoatia ajira anapomaliza elimu yake suala linalosaidia kupunguza matendo maovu hapa nchini.