Alhamisi , 9th Jul , 2015

Wanamichezo wawili wa Tanzania wanatarajia kujaribu bahati yao hapo kesho katika mashindano ya Dunia ya Vyuo vikuuu yaliyoanza Julai tatu mwaka huu nchini Korea.

Katika taarifa yake, Mwenyekiti wa michezo ya vyuo vikuu Tanzania TUSA, Noel Kihunsia amesema wanamichezo hao ambao ni Charles Msabila anayetarajia kushiriki mchezo wa kuogelea na Nice Antony atachuanja katika riadha.

Kihunsi amesema, Tanzania ina matumaini makubwa ya kuvuna medali katika mashindano hayo kutokana na kiwango kikubwa walichonacho kilichotokana na mazoezi ya muda mrefu waliyoyafanya hapa nchini.