Alhamisi , 12th Feb , 2015

Timu za taifa za kriketi kutoka nchi za Kenya, Uganda na Namibia zitawasili Tanzania leo kwa ajili ya michuani ya ligi ya ICC-Afrika Division 1 kwa wavulana chini ya miaka 19 itakayoanza Jumapili Dar es Salaam.

Afisa wa Chama Cha Kriketi Tanzania (TCA), Kazim Nasser amesema kuwa timu kutoka Botswana inategemewa kuwasili Jumatano jioni wakati timu ya Nigeria itawasili Ijumaa.

Kwa mujibu wa Nasser, maofisa wasimamizi wa michuano hiyo kutoka Afrika ya Kusini na Namibia pia watawasili mapema kabla ya mashindano kuanza.