Jumapili , 19th Jun , 2016

Wawakilishi wa klabu ya Bidvest ya Afrika Kusini wanatarajiwa kutua nchini wakati wowote kwa ajili ya mazungumzo na klabu ya Simba juu ya kiungo Jonas Mkude.

Mkude alikuwa Afrika Kusini mwaka jana kwa majaribio Bidvest na ikaripotiwa amefuzu, ingawa klabu hiyo haikujaribu kuzungumza na klabu yake.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema Mkude ameutaarifu uongozi wa Simba kuhusu ujio huo wa watu kutoka Afrika Kusini.

Hans Poppe amesema Simba haina desturi ya kumzuia mchezaji anapotakiwa na timu ya nje kwa sababu faida zake ni kama za Mbwana Samatta sasa anacheza Ulaya.