Jumapili , 2nd Feb , 2020

Mabingwa wa kihistoria nchini, klabu ya Yanga wanashuka dimbani leo kukabiliana na Mtibwa Sugar katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Mtibwa Sugar dhidi ya Yanga

Mtibwa Sugar inashuka dimbani ikiwa haijafanya vizuri katika ligi hivi karibuni tangu ilipotoka kushinda kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar, huku Yanga wakionekana kuimarika chini ya kocha Luc Eymael.

Kuelekea mchezo huo, Yanga itawakosa takribani wachezaji watatu ambao ni Mrisho Ngassa ambaye ana adhabu ya kukosa mechi tatu, sambamba na Ramadhan Kabwili pamoja na Anderw Vincent mwenye kadi tatu za njano, na katika upande wa Mtibwa itamkosa Dickson Job aliyepata kadi nyekundu kwenye mchezo dhidi ya Azam FC.

Msimu uliopita timu hizi zilipokutana kwa mara ya kwanza katika Uwanja wa Taifa, smbspo Yanga ilishinda mabao 2-1 na zilipokutana mzunguko wa pili katika Uwanja wa Jamhuri, Yanga ilifungwa bao 1-0.

Kwenye msimamo wa ligi, Yanga inashika nafasi ya sita ikiwa na pointi 28 baada ya kucheza mechi 15 na Mtibwa Sugar inakamata nafasi ya 10 ikiwa na pointi 23 baada ya kucheza mechi 17.