
Wanafainali ya michuano ya wazi ya mieleka iliyomalizika hivi karibuni jijini Dar es salaam katika ukumbi wa Msasani Beach ikishirikisha vilabu vinne vya Nevi, Jeshi Stars, Dar Combine na Ilala ,wameiomba serikali kuusaidia mchezo huo ili utangazike kimataifa.
Wanamieleka Hassan Mbaga na Bakari Mukeshi wamesema kuwa changamoto kubwa katika mchezo huo ni vifaa na udhamini katika maandalizi
Wachezaji hao wameongeza kusema kuwa mara nyingi wachezaji wanakua katika morali ya hali ya juu lakini wanakwamishwa na mambo hayo mawili likiwemo suala la vyama au klabu kukosa pesa kwaajili ya kugharimia timu.