
Mlinzi wa klabu ya soka ya Man City na timu ya taifa ya England Kyle Walker
Walker anatuhumiwa kuvunja sharti la 'lockdown' kwa kuonekana mitaani mara kadhaa, ambapo mara ya kwanza ilikuwa ni mwanzoni mwa Aprili alipoandaa sherehe nyumbani kwake na kualika watu.
Tayari tukio hilo lilishachukuliwa hatua za kinidhamu na klabu yake ya Man City, lakini kabla ya ligi kurejea ameripotiwa kuvunja sheria tena kwa kuonekana mitaani mara tatu kwa siku.
The Sun wameripoti kuwa jana Alhamisi Mei 7, 2020, Walker alionekana mtaani ambapo alikwenda kwa dada yake, kwa wazazi wake na kuendesha baiskeli mtaani na rafiki yake.
Mapema leo Walker amekiri kuwa alikwenda Sheffield kumtembelea na kumpelekea zawadi ya siku ya kuzaliwa dada yake na baadaye alikwenda kwa wazazi wake kuchukua chakula.
'Nimewaona ndugu zangu na mimi ni binadamu kila nachofanya kinapoelezwa tofauti naumia na familia yangu inaumia pia, nahisi sasa nadharirishwa'', ameeleza Walker.