Gulam Rashid (Aliyesimama) na baadhi ya viongozi wa TOC
kamisheni hiyo pia imewaondoa baadhi ya wagombea kutokana na kukosa sifa ndani ya kamati hiyo.
Katibu wa Kamisheni ya Uchaguzi ya kamati ya Olimpiki nchini TOC Harrison Chaulo amesema, mara baada ya kutangaza wagombea waliopitishwa na nafasi zao, wagombea hao wanatakiwa kuanza kampeni kuanzia leo na kuhitimisha siku moja kabla ya kuelekea katika uchaguzi ambao utafanyika Desemba 10 mwaka huu mjini Dodoma.
Chaulo amewataja waliopita katika mchakato huo kuwa ni:
Nafasi ya Urais: Gulam Rashid
Makamu: Henry Tandau
Katibu: Filbert Bayi
Naibu Katibu Mkuu: Suleiman Jabir
Mtunza Hazina: Charles Nyanga
Mtunza hazina Msaidizi: Juma Zaidy

Filbert bayi - Mgembea pekee katika nafasi ya ukatibu mkuu
Kamati ya utendaji Bara: Irene Mwasanga, Muharam Mchume, Noorelain Shariff, Noel Kihunsi, Amina Lyamaiga, Donath Massawe na Juliana Yassoda.
Kamati ya utendaji Zanzibar: Nasra Mohamed, Mussa Abdul-Rabi Fadhil, Suleiman Khamis, Abdulhakim Chasama, Ramadhan Omar, Said Mansab, Sheha Ali, Shukuru Nassor.
Amewataja wagombea ambao hawakupitishwa ni Hassan Jarufu ambaye hakuhudhuria usaili bila taarifa pamoja na fomu yake kusainiwa na chama ambacho si mwanachama wa TOC.
Lukelo Willilo aliyekuwa akiwania nafasi ya mwanakamati Bara: Fomu yake haikusainiwa na mhusika halisi.
Abdulrahman Hassan ambaye alikuwa akigombea nafasi ya mwanakamati Zanzibar ambaye pia ameondolewa katika ugombea kwa kutohudhuria usaili bila ya taarifa









