Hii ni mara ya pili kikosi hicho kukutana na Rais Magufuli baada ya ile ya mara kwanza kuwaita Oktoba 19, 2018 ambapo aliwakabidhi shilingi milioni 50, ikiwa ni sehemu ya hamasa kuelekea kufuzu kwenye fainali za michuani hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Gerson Msigwa imesema Rais Magufuli atakutana wachezaji hao leo Ikulu Jijini Dar es salaam, lengo ni kupata nao chakula cha mchana.
"Rais Magufuli leo Machi 25, 2019 atakutana na wachezaji wa Taifa Stars, Viongozi wa TFF, Kamati ya Uhamasishaji na Bondia Hassan Mwakinyo Ikulu DSM, atawapongeza na kula nao chakula cha mchana." imesema taarifa ya Msigwa.
Akiwakabidhi milioni 50 Oktoba 19, 2018 Rais Magufuli alisema, ''nawakabidhi shilingi milioni 50, nahodha wa Taifa Stars na Rais wa TFF mbele ya Waziri Mwakyembe hapa hapa muondoke nazo lakini mkashinde na zitumike vizuri kwa ajili ya wachezaji, msiposhinda niwaambie kabisa mtazitapika kwa namna nyingine''.







