Alhamisi , 26th Nov , 2015

Kocha mkuu wa timu ya vijana ya klabu ya Simba Niko Kiondo amesema timu hiyo bado ina nafasi ya kuweza kufanya vizuri kama wachezaji watajitambua wanapokuwa uwanjani.

Kiondo amesema, timu hiyo ni nzuri kama wachezaji watajituma ukiachia mapungufu yaliyo ndani ya timu hiyo ambayo pia yakifanyiwa kazi timu hiyo itazidi kuwa vizuri zaidi katika mechi mbalimbali za ligi kuu.

Kiondo amesema, kuna baadhi ya wachezaji kinachowasumbua ni upatikanaji wa nafasi katika timu kwani mpira ni uleule lakini wanachotakiwa ni mafunzo ya usikivu kwa wachezaji na kama watapatiwa nafasi katika timu wanaweza kucheza na kuipa faida timu.