Jumatano , 30th Mar , 2022

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema Serikali imejipanga kuwafadhili Waamuzi kwa kuwapeleka nje ya Nchi kupata mafunzo yatakayowaimirisha kujua vyema Sheria na Utaratibu wa Soka.

(Baadhi ya Waamuzi wa Ligi Kuu NBC Tanzania msimu wa mwaka 2021-22)

Waziri Mchengerwa pia amesema Serikali itaendeleza Elimu ya Uraia na Uzalendo kwa taifa letu ili kuondokana na vitendo vya rushwa na upendeleo michezoni vitu ambavyo ni kinyume na Maadili nchini.

''Licha ya kuwa TFF imekuwa ikiandaa semina mbalimbali na hata kuwafungia waamuzi takribani 13,sisi Serikali tTumeandaa mpango kazi kupitia asilimia 5 ambayo Mh. Rais ameitenga kupitia bajeti ya mwaka jana2021/2022 ambayo moja kwa moja itakwenda kutengeneza waamuzi wapya" aemsema Waziri Mchengerwa.

''Serikali tumejipanga kuhakikisha kwamba tunawafadhili Waamuzi wapya ambao watakwenda kusoma kama itakuwa ndani ya nchi kwenye chuo chetu cha Mallya tunachokijenga na Mh Rais wa nchi ametoa fedha za kutosha,lakini pia wapo Waamuzi tutawapeleka nje ya nchi kwenda kujifunza itakayowawezesha kuwa waamuzi wazuri watakaojua vyema sheria na taratibu lakini pia kuendeleza elimu ya uraia na uzalendo kwa taifa letu ili kuondokana na vitendo vya rushwa,upendeleo vitendo vilivyo kinyume na maadili'' alimalizia Waziri mwenye dhamana ya Michezo, Mchengerwa.