Jumanne , 15th Jun , 2021

ligi kuu soka Tanzania bara inarejea tena hii leo baada ya mapumziko ya takribani wiki mbili kupisha kalenda ya kimataifa ya FIFA ambapo timu za taifa zilikuwa zikicheza michezo ya kirafiki na za mashindano.

Wachezaji wa Biashara na Namungo wakiwania mpira kwenye moja ya michezo ya Ligi

Mchezo pekee leo unachezwa huko mkoani mara katika uwanja wa Karume ambapo Timu ya Biashara United Mara watakuwa wenyeji wa Namungo FC ya Mkoani Lindi, mchezo huu unachezwa Saa 10:00 Jioni.

Timu hizi zinatofautiana alama 4 kwenye msimamo wa ligi, Biashara wapo juu nafasi ya nne wakiwa na alama 45 wakiwa wamecheza micheza michezo 30 wakati Namungo wapo nafasi ya nane wakiwa na alama 41 katika michezo 30.

Mchezo wa mkondo wa kwanza timu hizi hazikufungana kwenye mchezo ambao ulichezwa Disemba 09, 2021 katika dimba la Majaliwa mkoani Lindi, na katika michezo mitatu ya ligi waliokutana wametoka sare michezo miwili na Biashara wameshinda mchezo mmoja.