Ijumaa , 2nd Oct , 2020

Michezo ya raundi ya tano ligi kuu soka Tanzania bara kuanza kuunguruma hii leo kwa mchezo mmoja utakao chezwa Jijini Dodoma ambapo klabu ya Dodoma Jiji FC watakuwa wenyeji wa Ruvu Shooting ya Pwani.

Dodoma jiji FC wameshinda michezo yote miwili waliocheza katika uwanja wa Jamhuri msimu huu

Dodoma Jiji wanarejea katika uwanja wao wa nyumbani wa Jamhuri baada ya kucheza michezo miwili ya ugenini ambapo walicheza dhidi ya Polisi Tanzania mchezo ambao walipoteza kwa mabao 3-0 lakini pia walitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Coastal.

Kikosi cha Dodoma chini ya kocha Mbwana Makata mpaka sasa kimekusanya jumla ya alama saba na alama sita kati ya hizo saba wamezipata katika uwanja wao wa nyumbani na wapo nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi.

Kikosi cha Ruvu Shooting kimefunga bao moja tu ambalo walifunga kwenye mchezo dhidi ya Gwambina mchezo amabo walishinda bao 1 -0, na ndo mchezo pekee walioshinda katika michezo minne huku wakiwa na sare katika michezo miwili na wamepoteza mchezo mmoja.

Chini ya kocha Charles Boniface Mkwasa Ruvu Shooting imekusanya jumla alama tano na kikosi hicho kipo nafasi ya kumi kwenye msimamo wa ligi.

Mchezo huu pekee wa ufunguzi wa michezo ya raundi ya tano kwa siku ya leo utachezwa Saa 10 Jioni.

Katika muendelezo wa michezo ya raundi ya tano siku ya Jumamosi itachezwa michezo minne, jumapili michezo mitatu na Jumatatu utachezwa mchezo mmoja.

Kesho Jumamosi

Gwambina FC Vs Ihefu FC

Namungo FC Vs Mwadui FC

Mbeya City FC Vs Tanznaia Prisons

Yanga SC Vs Coastal Union

Jumapili

Biashara United Vs Mtibwa Sugar

JKT Tanzania Vs Simba SC

Azam FC Vs Kagera Sugar

Jumatatu

KMC Vs Polisi Tanzania