Jumatatu , 11th Mei , 2020

Vilabu vya Premier League pamoja na mamlaka za soka nchini England wanakutana leo Mei 11, 2020 kujadili juu ya hatma ya msimu wa ligi wa 2019/20 kama inaendelea na msimu au vinginevyo.

Shughuli za urushaji matangazo kwenye moja ya mechi za Premier League

Hata hivyo Waziri Mkuu Boris Johnson katika hotuba yake jana Mei 10, hakuweka wazi kama michezo itarejeshwa rasmi lakini leo serikali pia huenda ikatoa mwelekeo mpya.

Chama cha soka nchini humo (FA) kilitoa pendekezo kwa vilabu kuwa mechi zinatakiwa zichezwe kwenye viwanja huru ili kuweza kumaliza mechi 92 zilizobaki ndani ya muda mzuri kabla ya kuanza kwa msimu ujao.

Hata hivyo mapendekezo hayo yanapingwa vikali na baadhi ya vilabu kutokana na kuhitaji kucheza nyumbani ili kuwa na faida ya uwanja wa nyumbani.

Vilabu ambavyo tayari vimeshaweka wazi kutounga mkono mapendekezo hayo ni Crystal Palace, Brighton na Aston Villa.

Baadhi ya ripoti zinaeleza kuwa Serikali ina mpango wa kuruhusu mazoezi yaanze kisha ligi kuu kuanza kuchezwa Juni 12, 2020.