Jumatano , 13th Mei , 2015

Chama cha mpira wa kikapu nchini TBF kimevitaka vilabu vya mpira wa kikapu nchini vizingatie mafunzo ya vijana zaidi kuliko kuendelea na watu wazima ili kukuza vipaji na kuongeza vipaji vya mchezo huo hapa nchini.

Akizungumza na East Africa Radio, Kamishna wa Ufundi wa TBF, Manase Zabloni amesema katika ligi hiyo inaonesha timu za Mabibo na Morogoro Young Stars ambazo zina vijana zinazidi kufanya vizuri zaidi katika ligi hiyo.

Manase amesema, timu zitakazoshika katika nafasi ya kwanza kwa upande wa wanawake na wanaume zitaweza kushiriki michuano ya kanda ya tano itakayofanyika Kampala Uganda Agosti mwaka huu kwa kushirikisha nchi za ukanda wa tano kwa Afrika.