Katibu mkuu wa JATA Innocent Malya amesema, chama chake kimeshindwa kulipa ushuru ili kuvikomboa vifaa hivyo hivyo kutokana na hali hiyo huenda vikapigwa mnada.
Malya amesema, wakiamua kuwaambia ukweli IJF kwamba wameshindwa kulipa ushuru ili vifaa viruhusiwe kutoka lakini pamoja na kuwashauri wavipeleke nchi nyingine kimejitokeza kikwazo kingine baada ya serikali kutaka vilipiwe deni wanalodaiwa ambapo IJF ilisaidia kwa kutoa milioni tatu pointi sita ambapo kiasi kilichobaki kilikuwa no milioni tisa pointi mbili ili viweze kutolewa.
Malya amesema, kinachoelekea kutokea safari hii kinafanana na kilichowahi kufanyika mwaka 2006 ambapo IJF ilitoa vifaa kwa JATA lakini vilikwama bandarini baada ya kukosekana kwa fedha za kulipia ushuru hatua iliyosababishwa vipigwe mnada.