Jumanne , 8th Jun , 2021

Kiungo wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Uholanzi Donny Van de Beek ameondolewa kwenye kikosi cha Uholanzi kitakachoshiriki michuano ya Euro 2020 kutokana na majeruhi.

Donny Van de Beek

Taarifa za majeruhi ya kiungo huyo zimetolewa leo asubuhi kupitia mtandao wa kijamii wa Tweeter, lakini pia taarifa hiyo iliweka wazi kuwa kocha Frank de Boer hatajaza nafasi inayoachwa na kiungo huyo kwenye kikosi hicha cha the Oranje.

Van de Beek alijiunga na Manchester United kwenye dirisha la usajili la majira ya joto lilopita akitokea Ajax ya nyumbani kwao Uholanzi, kwa ada ya uhamisho ya pauni million 35 ambayo ni zaidi ya bilioni 114 kwa pesa za kitanzania. Lakini hajawa na mwanzo mzuri katika viunga vya Old Traford kutokana na kutopewa nafasi ya kucheza mara kwa mara na kocha Ole Gunnar Solskjaer.

Uholanza imepangwa kundi C kwenye michuano hii pamoja na timu za Austria, Ukraine na Mecedonia ya Kaskazini na itacheza mchezo wake wa kwanza Juni 13, 2021 dhidi ya Ukraine.

Na ni kwa mara ya kwanza Oranje watakuwa wakishiriki mashindano makubwa tangu mwaka 2014, kwani walishindwa kufuzu kwenye mashindano makubwa yaliyopita, fainali za michuano ya Euro mwaka 2016 na Kombe la Dunia mwaka 2018.