Alhamisi , 26th Nov , 2015

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania Kilimanjaro Stars, Abdallah Kibadeni amesema wanaamini watashinda mechi zote za hatua ya makundi katika michuano ya Chalenji.

Kibadeni amesema pamoja na kuwa mechi ya mwisho ya makundi watamaliza na wenyeji Ethiopia hapo kesho, bado wanaamini watashinda mchezo huo.

Kibaden amesema wanajua mechi itakuwa ngumu zaidi kwa kuwa wanakutana na wenyeji lakini watahakikisha wanashinda kwani kikosi kitakuwa na imani zaidi imani kwa maana ya kujiamini kutokana na kushinda hali ambayo itasaidia katika mechi zijazo.

Stars imecheza mechi mbili za michuano ya Chalenji ikianza kwa kuitwanga Somalia kwa mabao 4-0 kabla ya kiivurumisha Rwanda kwa mabao 2-1 katika mechi ya pili.