Ijumaa , 4th Mar , 2022

Baada ya Jumatatu iliyopita vilabu vya soka vya Urusi pamoja na timu zake za taifa za nchi hiyo kusimamishwa rasmi kushiriki mashindano yote yaliyo chini ya shirikisho la soka barani ulaya UEFA na shirikisho la soka duniani FIFA,

(Wachezaji wa timu ya Taifa ya Urusi)

Shirikisho la Soka nchini Urusi limesema litakwenda Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) kukata rufaa dhidi ya kufungiwa kushiriki mashindano ya kimataifa baada ya nchi hiyo kuivamia Ukraine. hivyo urusi itafungua kesi dhidi ya shirikisho la soka duniani FIFA na soka barani ya Ulaya UEFA kutaka timu za taifa za wanaume na wanawake zirejeshwe kucheza mechi zao za kufuzu Kombe la Dunia kwa wanaume na timu ya wanawake iwekwe katika mashindano ya Euro 2022 nchini Uingereza.

(Rais wa FIFA Giann Infantino na Rais wa Urusi Vladmir Putin)

Shirkisho hilo pia limesema linaweza kuomba kusitishwa kwa mashindano ambayo awali walikuwa wamepangiwa kushiriki iwapo FIFA na UEFA watakataa rufaa yao. Taarifa ya mamlaka ya soka ya Urusi imesema inaamini kwamba Fifa na Uefa hazina mamlaka kisheria wakati wa kufanya maamuzi juu ya kuziondoa timu za Urusi kwenye mashindano yote.

Klabu ya Spartak Moscown ya Urusi imeondolewa katika Ligi ya Europa hivyo wapinzani wao RB Leipzig watatinga robo fainali moja kwa moja. Huku klabu ya RB Salzburg nayo ikiondolewa katika michuano ya ligi ya mabingwa ulaya na kuwapa nafasi Bayern Muchen kutinga hatua ya robo fainali moja kwa moja.